Thursday, 28 December 2017

USHAHIDI KIAKIOLOJIA YA KUZUNGUMZWA KISWAHILI KABLAYA UJIO WA WAGENI KATIKA UPWA A.MASHARIKI

      Ushahidi wa Akiolojia ni mbinu wanazotumia wanahistoria kuchunguza Tamaduni za watu katika vipindi tafauti vya historia kwa kuchunguza mabaki ya majengo na vitu mbalimbali katika ardhi.
     Wanakiakiolojia wanatafuta vitu vilivyobaki katika Ardhi  kwa mfano mabaki ya majengo,silaha,mbegu,vyombo,makaburi na mifupa ya watu.
      Ushahidi  wa  kiakiolojia  unathibitisha wazi kuzungumzwa kwa  Kiswahili  kabla  ya  kuja kwa  wageni  katika  mwambao wa Afrika ya mashariki kama ifuatavyo:
     Kugunduliwa kwa  miba  ya samaki, ushahidi huu unaonesha kuwa wakaazi wa  mwambao wa  Afrika ya mashariki kama  vile  Lamu,Kilwa walikuwa wakijishughulisha na shughuli za uvuvi, hivyo katika harakati zao  waliweza  kuwasiliana kwa kutumia lugha ya Kiswahili.  Ushahidi  wa hili   tunauona baada ya NEVILLE CHITTICK kufanya ugunduzi mwaka 800BK -1100BK.
     Kugunduliwa kwa vyungu vya kienyeji,kabla ya kuja kwa wageni Waswahili wa Mwambao, wa Afrika ya mashariki walijishughulisha na kazi ya kufinyanga vyungu ambavyo kwa wakati huo vilikuwa having’arishwi,hivyo kugunduliwa kwa mabaki ya vyungu katika mijiya Manda,Shanga Kilwa ambayo vilitumika katika miaka ya 800 hadi 1000 hivi vinaonesha kuwa kazi hii ilikuwa ni ya utamaduni wa waswahili,hivyo hata  lugha waliyokuwa wakiizungumza ni ya Kiswahili, hivyo inathibitisha kuwa Kiswahili kilitumika hata kabla ya kuja kwa wageni.
      Kugunduliwa kwa mashimo ya majengo,historia inatueleza kwamba kabla ya kuja kwa wageni katika mwambao wa Afrika ya mashariki,Waswahili waliishi katika nyumba zilizojengwa kwa miti nakukandikwa kwa udongo kama ni moja ya sehemu ya utamaduni wao,hivyo ushahidi wa kimachimbo uliofanywa na MARK KARTON katika mwaka 920-1020 amegunduwa mashimo yaliyokaa duara na mengine yaliyokaa mstatili kuashiria kwamba hapo awali Waswahili wa mwambao walijenga nyumba za miti na lugha iliyotumika ni Kiswahili.
       Kugunduliwa kwa shanga za simbi,vilevile kugunduliwa kwa shanga za simbi katika mwambao wa Afrika ya mashariki mfano katika maeneo ya Manda na Kilwa mnamo mwaka 800-1000 kunaonesha wazi kuwa Waswahili wa kimwambao walijishughulisha na utengenezaji wa shanga za simbi ambazo zilikuwa kama ni mapambo yao na hivyo kwasababu ya Utamaduni wao kuwa ndio huo basi na  lugha yao ikawa ni Kiswahili.
      Kugunduliwa kwa chuma, pia katika ushahidi wa Akiolojia uliofanywa na CHITTECK unabainisha wazi kuwa waswahili waliweza kugunduwa makapi ya chuma na wakaweza kuyeyusha na kufua chuma na kutengeneza Ndoana,vichwa vya Mishare na, hata Majembe na Shoka, hivyo vitu hivi ndiyo walivyovitumia katika maisha yao ya  kila siku, ambapo pia wanaashiria hata lugha waliyokuwa  wakizungumza ni Kiswahili.
       Kugunduliwa kwa Mbegu za Mtama ,ushahidi huu unaonesha kwamba waswahili wa mwambao wa Afrika ya mashariki walikuwa  wakijishughulisha na ukulima na hasa kilimo cha Mtama, na inaonesha kuwa waswahili huwo ulikuwa ndio utamaduni wao wa Kiswahili na hata lugha yao ikawa ni ya Kiswahili. CHITTECK anasema “Nao walikuwa wakulima katika wakati huo’’.
         Pia MARK KARTON ametenganisha vipindi 5 katika ukuwaji wa mji wa Shanga:
         850-920 safu hii ilionesha mabaki ya vyungu, mbeguza mtama, katika safu hii nyumba havikuwa bayana.
        920-1020  safu hii inaonesha majengo yaliyokaa duara na juu yake yapo ya mstatili yaliyokandikwa kwa udongo na kushikiliwa kwa fito.
       1020-1250 safu hii inaonesha matumizi ya matumbawe kushikiliwa kwa udongo katika msingi kisha pakajengwa nyumba ya miti iliyochanganywa na fito na kukandikwa kwa dongo.
          1250- 1320         Safu hii inaonesha chokaa ilitumika kujenga msikiti mzuri zaidi na paa lililojegwa kwa kutumia mbao.
          1320-1440 safu hii ilionesha matumizi ya paa za sleti, matumbawe,chokaa na mchanga zilitumika katika ujenzi wa nyumba.
        Kwa kupitia safu hizi kwa vipindi tafauti, pia inaonesha jinsi waswahili wa mwambao walivyokuwa na utamaduni wao wa  makaazi  na jinsi walivyokuwa na utaalamu wa kusanifu makazi yao,na hii inaonesha hata lugha yao ya mawasiliano ni Kiswahili kwa wakati huo.
       Hivyo basi ushahidi wa Kiakiolojia nao unatusaidia katika kutupatia mfuatano bayana wa tarehe kuhusu maendeleo ya awali ya watu waliokuwa wanazungumza Kiswahili katika mwambao wa Afrika ya mashariki hata kabla ya kuja kwa wageni.
                    














waswahili wa pwani


MASHAIRI YA PWANI