Ushahidi wa Akiolojia
ni mbinu wanazotumia wanahistoria kuchunguza Tamaduni za watu katika vipindi
tafauti vya historia kwa kuchunguza mabaki ya majengo na vitu mbalimbali katika
ardhi.
Wanakiakiolojia
wanatafuta vitu vilivyobaki katika Ardhi
kwa mfano mabaki ya majengo,silaha,mbegu,vyombo,makaburi na mifupa ya
watu.
Ushahidi wa
kiakiolojia unathibitisha wazi
kuzungumzwa kwa Kiswahili kabla
ya kuja kwa wageni
katika mwambao wa Afrika ya
mashariki kama ifuatavyo:
Kugunduliwa kwa miba
ya samaki, ushahidi huu unaonesha kuwa wakaazi wa mwambao wa
Afrika ya mashariki kama
vile Lamu,Kilwa walikuwa
wakijishughulisha na shughuli za uvuvi, hivyo katika harakati zao waliweza
kuwasiliana kwa kutumia lugha ya Kiswahili. Ushahidi
wa hili tunauona baada ya
NEVILLE CHITTICK kufanya ugunduzi mwaka 800BK -1100BK.
Kugunduliwa kwa vyungu
vya kienyeji,kabla ya kuja kwa wageni Waswahili wa Mwambao, wa Afrika ya
mashariki walijishughulisha na kazi ya kufinyanga vyungu ambavyo kwa wakati huo
vilikuwa having’arishwi,hivyo kugunduliwa kwa mabaki ya vyungu katika mijiya
Manda,Shanga Kilwa ambayo vilitumika katika miaka ya 800 hadi 1000 hivi
vinaonesha kuwa kazi hii ilikuwa ni ya utamaduni wa waswahili,hivyo hata lugha waliyokuwa wakiizungumza ni ya
Kiswahili, hivyo inathibitisha kuwa Kiswahili kilitumika hata kabla ya kuja kwa
wageni.
Kugunduliwa kwa mashimo
ya majengo,historia inatueleza kwamba kabla ya kuja kwa wageni katika mwambao
wa Afrika ya mashariki,Waswahili waliishi katika nyumba zilizojengwa kwa miti
nakukandikwa kwa udongo kama ni moja ya sehemu ya utamaduni wao,hivyo ushahidi
wa kimachimbo uliofanywa na MARK KARTON katika mwaka 920-1020 amegunduwa
mashimo yaliyokaa duara na mengine yaliyokaa mstatili kuashiria kwamba hapo
awali Waswahili wa mwambao walijenga nyumba za miti na lugha iliyotumika ni
Kiswahili.
Kugunduliwa kwa shanga
za simbi,vilevile kugunduliwa kwa shanga za simbi katika mwambao wa Afrika ya
mashariki mfano katika maeneo ya Manda na Kilwa mnamo mwaka 800-1000 kunaonesha
wazi kuwa Waswahili wa kimwambao walijishughulisha na utengenezaji wa shanga za
simbi ambazo zilikuwa kama ni mapambo yao na hivyo kwasababu ya Utamaduni wao
kuwa ndio huo basi na lugha yao ikawa ni
Kiswahili.
Kugunduliwa kwa chuma,
pia katika ushahidi wa Akiolojia uliofanywa na CHITTECK unabainisha wazi kuwa
waswahili waliweza kugunduwa makapi ya chuma na wakaweza kuyeyusha na kufua
chuma na kutengeneza Ndoana,vichwa vya Mishare na, hata Majembe na Shoka, hivyo
vitu hivi ndiyo walivyovitumia katika maisha yao ya kila siku, ambapo pia wanaashiria hata lugha
waliyokuwa wakizungumza ni Kiswahili.
Kugunduliwa kwa Mbegu
za Mtama ,ushahidi huu unaonesha kwamba waswahili wa mwambao wa Afrika ya
mashariki walikuwa wakijishughulisha na
ukulima na hasa kilimo cha Mtama, na inaonesha kuwa waswahili huwo ulikuwa ndio
utamaduni wao wa Kiswahili na hata lugha yao ikawa ni ya Kiswahili. CHITTECK
anasema “Nao walikuwa wakulima katika wakati huo’’.
Pia MARK KARTON
ametenganisha vipindi 5 katika ukuwaji wa mji wa Shanga:
850-920 safu hii
ilionesha mabaki ya vyungu, mbeguza mtama, katika safu hii nyumba havikuwa
bayana.
920-1020 safu hii inaonesha majengo yaliyokaa duara na
juu yake yapo ya mstatili yaliyokandikwa kwa udongo na kushikiliwa kwa fito.
1020-1250 safu hii
inaonesha matumizi ya matumbawe kushikiliwa kwa udongo katika msingi kisha
pakajengwa nyumba ya miti iliyochanganywa na fito na kukandikwa kwa dongo.
1250- 1320 Safu hii inaonesha chokaa ilitumika
kujenga msikiti mzuri zaidi na paa lililojegwa kwa kutumia mbao.
1320-1440 safu hii
ilionesha matumizi ya paa za sleti, matumbawe,chokaa na mchanga zilitumika
katika ujenzi wa nyumba.
Kwa kupitia safu hizi
kwa vipindi tafauti, pia inaonesha jinsi waswahili wa mwambao walivyokuwa na
utamaduni wao wa makaazi na jinsi walivyokuwa na utaalamu wa kusanifu
makazi yao,na hii inaonesha hata lugha yao ya mawasiliano ni Kiswahili kwa
wakati huo.
Hivyo basi ushahidi wa
Kiakiolojia nao unatusaidia katika kutupatia mfuatano bayana wa tarehe kuhusu
maendeleo ya awali ya watu waliokuwa wanazungumza Kiswahili katika mwambao wa
Afrika ya mashariki hata kabla ya kuja kwa wageni.