Thursday, 28 December 2017
MAENDELEO YA KISWAHILI KATIKA ELIMU NA MAWASILIANO
Lado (1064), Lugha ni chombo cha mawasiliano baina ya binaadamu katika jumuiya fulani.
Potta (1960), Lugha ninutaratibu wa alama za sauti zilizopangiliwa kutokana na mazoea au matamshi ya watu kwa njia ya sauti, ambazo wanaadamu wanapelekeana habari na wanasikilizana.
TUKI(2004), Lugha ni mpangilio wa sauti na maneno unaoleta maana ambao hutumiwa na watu wataifa au kundi Fulani kwa ajili ya kuwasiliana.
Lugha ya Kiswahili ni lugha ambayo inatumiwa na watu wenye utamaduni na asili ya upwa wa pwani ya Afrika Mashariki katika shughulizao za kila siku.
Hivyo kutokana na kunea na maendeleo ya Kiswahili, sasa inaonekana lugha ya Kiswahili kuwa na watumiaji wengi zaidi ndani na nje ya Afrika Mashariki, kupelekea lugha hii ya Kiswahili kupata nafasi ya tano kutoka ya saba katika lugha bora za Ulimwenguni.
Hata hivyo,kutokana na hatua hii kubwa ya lugha ya Kiswahili, tayari kimekwishakubaliwa katika matumizi mbalimbali yakiwemo ya kielimu na kimawasiliano nje ya Afrika Mashariki. Kwa kuanzia na mafanikio ya lugha ya Kiswahili katika elimu kama ifuatavyo:-
Kuanzishwa kwa vyuo mbali mbali ambavyo vinafundisha lugha ya Kiswahili. Kiswahili kimefanikiwa duniani kupitia harakati mbalimbali za elimu ambapo Kiswahili kimepata fursa ya kufundishwa katika vyuo mbalimbali,ikiwemo marekani amboyo inaongoza kwa kuwa na vyou vikuu 50 ambavyo vinafundisha lugha hii ya Kiswahili.Mfano wa vyuo hivyo ni Harverd Universuty, Massachusetts Institute of Technology, Starnford University, University of Oxford na University of Cambradge ambavyo vinapatikana Marekani na Uingereza.
Pia, kuundwa kwa idara mbalimbali ambazo zinazoshughulikia zaidi ukuzaji na matumizi ya Kiswahili.Nje ya Afrika Mshariki lugha ya Kiswahili imefanikiwa kielimu kwa kuanzishwa kwa taasisi na idara nyingi ambazo zimepewa jukumu la kushughulikia ukuzaji na matumizi ya Kiswahili. Miongoni mwa idara hizo ni idara ya lugha na fasihi za kiafrika katika chuo kikuu cha Wistonsin U.S.A,idara ya masomo ya kiafrika kozi ya sanaa na sayansi ya jamii katika chuo kikuu cha Brunswikk U.S.A, Taasisi ya masomo ya lugha na utamaduni wa Ulaya na Afrika- Japan na Idara ya Kiswahili katika chuo kikuu cha masomo ya kigeni Haunkuk-Korea.
Vilevile, Kiswahili kimekwisha kubaliwa kutumika katika shirika la umoja wa mataifa linaloshughulikia elimu,sayansi na utamaduni. Lugha ya Kiswahili kimefanikiwa nje ya Afrika Mashariki katika elimu, kwa kukubalika matumizi ya lugha Kiswahili katika shirika hilo la umoja wa mataifa ambalo ni chombo muhimu sana katika elimu ambacho ni UNESCO.
Kuengezeka kwa watu kutoka mataifa mbalimbali.Watu kutoka mataifa mbalimbali ya Ulaya,Amerika na Asia kuja Afrika Mashariki kwa ajlil ya kujifunza lugha ya Kiswahili na kufanya tafiti mbalimbali zinohusiana na lugha ya Kiswahili ikwa ni moja ya mafanikio ya lugha ya Kiswahili.
Tukiachana na mafanikio haya ya kielimu pia kwa upandewa kimawasilino kuna mafanikio kadhaa ya lugha ya Kiswahilikama vile:-
Kwa upande wa maendeleo ya mtandao wa Intaneti .Kwa kiasi kikubwa imefanikisha juhudi za kukuza na kueneza Kiswahili duniani, hasa kupitia matumizi mbalimbali katika mtandao huo,wataalamu,wanasiasa na pamoja na watu mbalimblia wanatumia muda mwingi katika kuwasiliana, kutoa habari na hata kujifuna mengi katika mtandao kupitia progranu mtandaoni, katika injini pekuzi na kwabahati njema harakati zote hizo kwa sasa tunazipata kwa 100% kupitia lugha ya Kiswahili. Jambo ambalo hupelekea watu wengi kutumia chombo hicho kwa wakati mmoja na kuzidi kutumia mawanda ya utumizi wa lugha ya Kiswahili duniani kote.kwa mfano kupitia google injin unaweza ukasachi kwa kutumia lugha ya Kiswahili.
Pamoja na hayo, matumizi ya lugha ya Kiswahili katika vyombo vya habari kama vile redio, runinga na magazeti yamaendelea kuipa nguvu lugha ya Kiswahili. Hasa kwa kuongeza mara dufu vituo vya kutolea habari ambapo kupitia redio mbalimbali za kimataifa, zimekuwa zikitoa habari na matangazo yake katika lugha ya Kiswahili.Kwamfano wa vyombo vya habari hivyo ni sauti ya Amerika,shirika la utangazaji la Uingereza (BBC), sauti ya Ujerumani (DW), idhaa ya Kiswahili ya china na hata idhaa ya Kiswahili ya Jamuhuri ya Kiislamu ya Iran. Ambapo Kiswahili kimefikia kiwango cha juu kabisa cha kusikika , kwani sasa vinasikika dunia nzima.
Ama kwa upande wa Magazeti nayo pia yanachukua nafasi kubwa katika kuunga mkono juhudi za kukuza na kuendeleza lugha ya Kiswahili duniani, ambapo magazeti mbali mbali hasa ya Ujerumani yanaelezwa kwa Kiswahili na baadhi ya magazeti hayo ni kama vile Die tagseitung, Haneidelsbatt, Die Zeit, De tage speagal na mengineyo.
Kwa ujumla, kutokana na dondoo na maelezo ya hapo juu yanadhihirisha kuwa lugha ya Kiswahili inalingana sana katika elimu na mawasiliano nje ya Afrika Mashariki,hivyo hali hii inapelekea lugha ya Kiswahili kupanda chati na hadhi kubwa zaidi ulimwenguni.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment