A) Kiswahili,
Kiswahili lugha inayozungumzwa maeneo mbalimbali ya pwani ya Afrikaya mashariki pamoja na maeneo mengine mbalimbali ya Afrika.Lugha hii inamchanganyiko mkubwa wa msamiati kutoka lugha nyengine mbalimbali zilizokutana kimawasiliano na lugha hii.kama vile kiarabu,kihindi,kireno,kijerumani na kiengereza.
B)
Waswhili,
Waswhili ni wenyeji wa mwambao wa afrika ya mashariki ambao lugha yao ya asili ni kiswahili,watu hawa na utamaduni wao wanajitafautisha na ule wa watu wengine katika baadhiya vipengele vya maisha,kama vile mavazi,malazi,malezi,dini na shughuli nyengine za kiuhumi,
Uswahilini,
uswahilini ni eneo maalum la kijografia lililoanzia somalia upande wa kaskazini na kuishia upande wa kusini pamoja na visiwa vilivyomo katika eneo hilo la mwamao ya afrika ya mashariki.
D)
Uswahili,
Ni utamaduni maalum wa waswahili unaoonekana katika matendo na maeneo ya waswahili wenyewe
TANBIHI:
Dhana ya mswahili,uswahili na uswahilini zimepotoshwa.kutoka uhalisia wake kuwa;
Mswahili: ni mtu mdanganyifu,laghai namropokaji.
Uswahilini: maeneo ya watu wajinga,ovyo,na wasio na mpangilio maalum wa hata ya makaazi yao.
Uswahili: Ni upuuzi, ujinga, ukale, unyama wa mawazo na maradhi ya kishirikina
No comments:
Post a Comment